ππππ ππ ππ
πππ ππ ππππππ ππ πππππππππππ ππππππππ ππππππππππ πππππ πππππππ ππ ππππππππ ππ ππππππ.
Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD), ikiongozwa na Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bi. Rehema Katuga, imepokea ujumbe kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa lengo la kujengeana uwezo kwenye masuala ya uandishi wa sheria na ujenzi wa mfumo wa uandishi wa sheria, jijini Dodoma.
Bi. Rehema, wakati wa ukaribisho amesema kuwa kuanzishwa kwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kumerahisisha upatikanaji wa sheria kwa wananchi na hii inasaidia katika upatikanaji wa haki.
"Tokea kuanzishwa kwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria imerahisha upatikanaji wa sheria kiurahisi kwa wananchi kwa kuwezesha kutoa toleo la urekebu wa sheria ambapo toleo la mwisho lilitolewa 2002, lakini pia imerahisisha upatikanaji wa sheria kwa lugha ya kiswahili na kiingereza kulingana na mahitaji," amesema Bi. Rehema.
Bi. Rehema ameendelea kwa kueleza kuwa kabla ya kutoa sheria kwa wananchi huwa zinapitia hatua za uhakiki ubora kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata sheria zilizo bora bila makosa yoyote.
"Kubwa ambalo tumefanya kama ofisi ni kuwa na kitengo cha uhakiki ubora kama unavyojua mlaji wa mwisho wa sheria ni mwananchi na kitengo kina jukumu la kuhakiki ubora wa sheria na tathmini ya sheria ili kubaini sheria zilizotungwa na bunge zinatimiza lengo la kutungwa kwakwe na kama kuna changamoto za uandishi wanaweza kuzishughuliki," ameeleza Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria.
Bi. Rehema ameeleza kuwa OCPD ipo katika hatua za ujenzi wa mfumo wa uandishi wa Sheria ambao utawezesha kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa uandishi wa sheria.
"Kwa sasa tupo katika hatua za kutengeneza mfumo wa uandishi wa sheria ili kuweza kutatua changamoto ambazo zinajitokeza wakati wa uandishi, ambapo itatusaidia kudumisha viwango vya uandishi wa sheria na kupunguza makosa yanayojitokeza wakati wa uandishi.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Uchambuzi wa Sheria na Miswada kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Bw. Saleh Mubarak ameshukuru kwa mapokezi mazuri kutoka kwa OCPD.
"Tunashukuru kwa mapokezi haya mazuri na tunatarajia kujifunza mengi haswa kwenye kutengeneza mfumo kwani na sisi tupo katika hatua za kutengeneza mfumo wetu utakaorahisha utekelezaji wa majukumu yetu," amesema Bw. Saleh.
