Majukumu ya Divisheni ya Uandishi wa Sheria
Majukumu ya Divisheni ya Uandishi wa Sheria
Divisheni inaongozwa na Mkurugenzi na ina Sehemu zifuatazo:
- Sehemu ya Uandishi wa Sheria Kuu; na
- Sehemu ya Uandishi wa Sheria Ndogo.
Lengo
Kuongeza ubora wa miswada na sheria.
Majukumu
Divisheni inatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kushauri kuhusu mapendekezo ya sheria kutoka kwenye wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali, mamlaka za serikali za mitaa, na taasisi nyingine za serikali.
- Kuhakiki na kutoa maoni ya kisheria kuhusu nyaraka za Baraza la Mawaziri kwa Mwandishi Mkuu wa Sheria.
- Kutekeleza maelekezo ya uandishi wa sheria kwa kuzingatia maamuzi ya Baraza la Mawaziri.
- Kushauri kuhusu kalenda ya utungaji wa sheria kwa kila wizara kwa kila mwaka wa fedha.
- Kuratibu na kuwezesha ushiriki na uwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge.
- Kuandaa ripoti juu ya masuala yanayotokana na Kamati ya Katiba, Sheria na Masuala ya Bunge na vikao vya Bunge.
- Kuandaa na kupitia nyenzo na zana za uandishi wa sheria.
- Kumshauri Mwandishi Mkuu wa Sheria juu ya utekelezaji wa maelekezo ya Baraza la Mawaziri na Bunge.
- Kuratibu mikutano ya wadau wakati wa mchakato wa uandishi wa sheria.
- Kuandaa, kupitia na kuwezesha kuchapishwa kwa sheria ndogo katika Gazeti la Serikali.
- Kuhakiki hati zote za kisheria zilizowasilishwa na wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, mamlaka za serikali za mitaa, na taasisi nyingine za serikali kwa ajili ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.
- Kuandaa, kutunza na kuhifadhi rejesta za miswada na sheria.
- Kushiriki katika uandishi wa sheria na hati za kisheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki na jumuiya nyingine za kikanda ambazo Jamhuri ya Muungano ni mwanachama.
- Kutoa mwongozo na msaada kwa wizara katika maandalizi na uwasilishaji wa nyaraka zinazohitajika kuwasilishwa kwa Baraza la Mawaziri au Bunge.
- Kuandaa hati za kisheria kwa ajili ya kuridhiwa na Bunge.
- Kushauri na kusimamia uchapishaji wa sheria kuu katika Gazeti la Serikali.