Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
.
Kitengo kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani.
Lengo
Kukuza utawala bora na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za ofisi kupitia usimamizi bora wa vihatarishi na kuboresha udhibiti.
Majukumu
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa Mpango Mkakati wa Ukaguzi na Mpango wa Ukaguzi wa Mwaka.
- Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uainishaji na utengaji sahihi wa akaunti za mapato na matumizi.
- Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uthabiti na ukamilifu wa taarifa za kifedha na kiutendaji.
- Kuandaa taarifa za kifedha na ripoti nyingine.
- Kupitia na kutoa taarifa kuhusu mfumo uliopo wa kulinda mali na kuthibitisha uwepo wa mali hizo.
- Kukagua na kutoa taarifa kuhusu utoshelevu wa mifumo ya udhibiti inayofanya kazi.
- Kukagua na kutoa taarifa kuhusu miradi iliyotekelezwa.
- Kuanzisha na kuendeleza rejesta ya vihatarishi.
- Kutoa taarifa ya usimamizi wa vihatarishi vilivyobainishwa kwa Kamati ya Vihatarishi na Ukaguzi, na kutoa mapendekezo ya kuboresha shughuli kuhusiana na ufanisi na utendaji bora.
- Kutathmini usalama wa tarifa na utayari wa taasisi kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yake na vihatarishi vinavyohusiana na changamoto hizo.
- Kutathmini na kutoa uthibitisho stahiki kama mifumo ya usimamizi wa vihatarishi, udhibiti na usimamizi inafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
- Kupitia na kutoa tarifa ya majibu ya menejimenti kuhusu ripoti za ukaguzi wa ndani, na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
- Kutoa taarifa kuhusu uzingatiaji wa taratibu za kifedha na kiutendaji zilizoainishwa katika sheria husika, kanuni na maelekezo ya udhibiti wa matumizi.
- Kuweka taratibu za ukaguzi ili kuwezesha mapitio na ukaguzi unaozingatia viwango vya kimataifa.