Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

Majukumu ya Kitengo cha Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu

.

Kitengo kinaongozwa na Mkurugenzi.

Lengo

Kutoa utaalam juu ya usimamizi wa rasilimaliwatu na masuala ya utawala.

Majukumu

Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kutafsiri Kanuni za Utumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu, na Sheria nyingine za Kazi.
  2. Kusimamia maadili na kuhamasisha shughuli zinazoongeza thamani kwa watumishi.
  3. Kumshauri Afisa Masuuli kuhusu masuala yanayohusiana na rasilimali watu na utawala.
  4. Kuhakikisha usimamizi na matumizi bora, yenye ufanisi na tija wa rasilimali watu.
  5. Kuratibu utekelezaji wa malengo ya taasisi kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja na timu.
  6. Kuwezesha mafunzo ya watumishi na maendeleo ya taaluma.
  7. Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi, na kusambaza takwimu na taarifa zinazohusiana na mipango ya maendeleo ya rasilimali watu.
  8. Kutoa takwimu na kusasisha kumbukumbu za taarifa mbalimbali za rasilimali watu.
  9. Kuratibu Baraza la Wafanyakazi.
  10. Kuratibu utatuzi wa malalamiko.
  11. Kuwezesha mahusiano ya wafanyakazi na ustawi wao, ikiwemo afya na usalama kazini, michezo na utamaduni.
  12. Kutoa huduma za kumbukumbu, usafirishaji wa nyaraka na mizigo.
  13. Kushughulikia masuala ya itifaki.
  14. Kuwezesha upatikanaji wa huduma za ulinzi, usafiri, na mahitaji ya jumla.
  15. kuwezesha matengenezo ya vifaa vya ofisi, majengo na maeneo ya ofisi.
  16. Kuratibu utekelezaji wa masuala anuwai.
  17. Kuratibu utekelezaji wa ushiriki wa sekta binafsi, maboresho ya mchakato wa kazi, na Mkataba wa Huduma kwa Wateja.
  18. Kuandaa taarifa za utendaji.