Misingi
.
1. Uadilifu
Tunazingatia uaminifu, kanuni thabiti za maadili na bidii katika kuhudumia taifa. Daima tunajitahidi kuzingatia kanuni za utawala bora.
2. Utaalamu
Tumejitoa katika kuhakikisha kuwa viwango vya juu vya ujuzi, maarifa na umahiri vinatumika na watumishi wote katika utekelezaji wa majukumu yao.
3. Ushirikiano
Tunahakikisha kuwa tunahusisha na kushirikisha wadau mbalimbali katika kutimiza majukumu yetu.
4. Uwazi na Uwajibikaji
Tunathamini uwazi, uaminifu na uwajibikaji kwa kila mtumishi katika kutekeleza majukumu ya OCPD. Kila mtumishi anatakiwa kukamilisha majukumu kwa wakati, kufanikisha matarajio ya utendaji, kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine na kudumisha tija na ufanisi.
5. Upatikanaji
Tunahakikisha kuwa sheria zote zilizoandikwa, zilizotafsiriwa, zilizorekebiwa na nyaraka nyingine za kisheria zilizoandaliwa kwa ajili ya kuridhiwa zinapatikana kwa urahisi.