Majukumu ya Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji
Majukumu ya Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji
.Kitengo kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo.
Lengo
Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango na bajeti.
Majukumu
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kumshauri Afisa Masuuli juu ya masuala yote yanayohusiana na ufuatiliaji, tathmini na utendaji.
- Kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Mwaka na Mpango Mkakati wa Kati.
- Kuanzisha na kuendeleza mfumo wa ufuatiliaji na tathmini.
- Kukusanya, kujifunza, kuelewa na kuchambua takwimu kwa ajili ya uundaji wa mipango na programu.
- Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya kuimarisha mchakato wa ufuatiliaji na tathmini.
- Kuratibu mapitio ya utendaji wa katikati ya mwaka na mwaka mzima.
- Kuimarisha uwezo wa ndani wa Ofisi katika masuala ya ufuatiliaji na tathmini kupitia mafunzo husika na uhamasishaji.
- Kuratibu Mikataba ya Utendaji kwa ajili ya Ofisi.
- Kufanya mapitio ya utekelezaji wa mipango na bajeti kwa ajili ya kufanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa sahihi.
- kuandaa na kuwasilisha taarifa za utendaji kwa Mwandishi Mkuu wa Sheria.