Majukumu ya Kitengo cha Fedha na Uhasibu
Majukumu ya Kitengo cha Fedha na Uhasibu
Kitengo kinaongozwa na Mhasibu Mkuu.
Lengo
Kutekeleza mifumo na taratibu za usimamizi wa fedha zinazoendana na taratibu na viwango bora vya uhasibu vinavyokubalika.
Majukumu
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kumshauri afisa masuuli juu ya masuala yote yanayohusiana na fedha na uhasibu.
- Kuandaa taarifa za fedha.
- Kupitia na kuendeleza mifumo ya uhasibu inayoendana na viwango vya fedha na utendaji.
- Kupitia na kutunza mifumo na taratibu za usimamizi wa fedha.
- Kulinda mali na rasilimali nyingine muhimu za fedha.
- Kuandaa na kufuatilia viashiria muhimu vya kifedha.
- Kuandaa na kutekeleza mfumo madhubuti wa udhibiti wa ndani unaosaidia uendelevu.
- Kutunza taarifa zote za madai ya ofisi na kuwezesha urejeshaji wa madai kwa wakati.
- Kuandaa taarifa za fedha za kila mwezi na robo mwaka.
- Kuanzisha na kutunza rejesta ya mali.
- Kusimamia taarifa ya matumizi ya mapato na hesabu.
- Kutunza kitabu cha fedha.
- Kupatanisha taarifa, taarifa za benki n.k.
- Kusimamia fedha.
- Kusimamia mapato kwa kuzingatia kanuni na taratibu za fedha zilizoainishwa.
- Kuandaa, kupitia na kufuatilia utekelezaji wa miongozo ya uhasibu.
- Kutunza kumbukumbu za pensheni.
- Kufuatilia mgao wa fedha na matumizi.