Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
.
Kitengo kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi.
Lengo
Kutoa utaalamu katika huduma za ununuzi na ugavi.
Majukumu
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kumshauri Afisa Masuuli kuhusu masuala yote yanayohusiana na ununuzi.
- Kusimamia shughuli zote za ununuzi na uondoshaji kwa njia ya zabuni isipokuwa uamuzi wa zabuni na utoaji wa mkataba.
- Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zabuni.
- Kupendekeza manunuzi na uondoshaji kwa taratibu za zabuni.
- Kuratibu utayarishaji wa taarifa za mahitaji.
- Kuandaa nyaraka za zabuni.
- Kuandaa matangazo ya fursa za zabuni.
- Kuandaa na kutoa nyaraka za mikataba zilizosainiwa.
- Kutunza taarifa za ununuzi kwa ajili ya kumbukumbu na taratibu za uondoshaji.
- Kutunza orodha au rejesta ya mikataba yote iliyotolewa.
- Kuandaa na kuwasilisha kwa menejimenti taarifa za robo mwaka za utekelezaji wa mpango wa ununuzi wa mwaka.
- Kuandaa na kutekeleza mpango wa ununuzi wa mwaka.
- Kufuatilia uzingatiaji wa mchakato na taratibu za ununuzi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
- Kusimamia na kufuatilia ununuzi wa vifaa vya ofisi.
- Kuendeleza na kusasisha orodha ya bidhaa na vifaa.
- Kufanya kazi kama sekretarieti ya bodi ya zabuni.
- Kuandaa vigezo msawazo au viwango vya huduma na bidhaa zinazonunuliwa na kuzingatia thamani ya fedha.
- Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utendaji kwa Mwandishi Mkuu wa Sheria.