Majukumu ya Divisheni ya Urekebu wa Sheria, Utafiti na Mafunzo
Majukumu ya Divisheni ya Urekebu wa Sheria, Utafiti na Mafunzo
Divisheni inaongozwa na Mkurugenzi na ina Sehemu mbili zifuatazo:
- Sehemu ya Urekebu wa Sheria Kuu; na
- Sehemu ya urekebu wa Sheria Ndogo.
Lengo
Kufanya urekebu wa sheria, utafiti wa kisheria na mafunzo.
Majukumu
Divisheni inatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kushauri kuhusu mapendekezo ya urekebu wa sheria kutoka katika wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, serikali za mitaa na taasisi nyingine za serikali.
- Kufanya urekebu wa sheria.
- Kuandaa toleo la urekebu la sheria za Tanzania katika vipindi vilivyoainishwa.
- Kuandaa toleo la mwaka la sheria zilizorekebiwa.
- Kuratibu utangazaji wa matoleo ya urekebu wa sheria.
- Kuratibu usambazaji wa toleo la urekebu wa sheria kwa kushirikiana na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali.
- Kujumuisha na kuunganisha sheria kuu na sheria ndogo zote.
- Kuandaa fahirisi na upangaji wa sura za sheria.
- Kuratibu mikutano ya ushirikishaji wadau wakati wa mchakato wa urekebu wa sheria.
- Kusimamia uchapishaji wa sheria zilizorekebiwa.
- Kushirikiana na Nchi Nyingine, ikiwa ni pamoja na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, katika kufanya utafiti wa masuala ya urekebu wa sheria na kupata taarifa nyingine muhimu zinazohusu usimamizi wa masuala ya urekebu wa sheria.
- Kuandaa na kutekeleza mpango wa urekebu wa sheria kwa kila mwaka wa fedha.
- Kuandaa, kutunza na kuendeleza rejesta ya sheria zilizorekebiwa.
- Kuandaa na kupitia nyenzo na zana za kufanyia urekebu wa sheria.
- Kuratibu na kusimamia shughuli za Divisheni za Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria.
- Kubaini maeneo ya utafiti na kufanya utafiti wa kisheria wa ndani kwa kushirikisha au bila kushirikisha wadau.
- Kuandaa ripoti za kisheria, maandiko, majarida, makala, maoni na mawasilisho ya semina na mikutano yanayohusiana na majukumu ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria.
- Kushauri na kusimamia uchapishaji wa sheria zilizorekebiwa katika Gazeti la Serikali.
- Kupitia miswada na sheria zilizochapishwa na kushauri juu ya masahihisho au maelezo, kama itakavyohitajika.
- Kuandaa na kutekekeleza Sera na Mpango wa Mafunzo.
- Kuratibu na kutoa mafunzo kuhusu uandishi wa sheria na nyanja nyingine zinazohusiana na uandishi wa sheria.
- Kukuza na kuhakikisha usahihi na mfanano katika sheria zilizorekebiwa kwa kuzingatia kanuni za uandishi wa Sheria.
- Kuendeleza maktaba ya sheria katika viwango stahiki.