Majukumu ya Divisheni ya Ufasiri wa Kisheria
Majukumu ya Divisheni ya Ufasiri wa Kisheria
.
Divisheni inaongozwa na Mkurugenzi na ina Sehemu mbili (2) zifuatazo:
- Sehemu ya Ufasiri wa Sheria Kuu; na
- Sehemu ya Ufasiri wa Sheria Ndogo.
Lengo
Kutoa huduma zinazohusiana na tafsiri ya sheria na tafsiri ya hati nyingine za kisheria.
Majukumu
Divisheni hii inatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kushauri wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi nyingine za serikali kuhusiana na masuala ya tafsiri za kisheria.
- Kutafsiri sheria na hati za kisheria kutoka lugha ya Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza na kinyume chake.
- Kutafsiri hati nyingine za kisheria katika lugha nyingine yoyote inayohitajika.
- Kuhakiki sheria zilizotafsiriwa.
- Kuandaa na kupitia nyenzo na zana za tafsiri ya sheria.
- Kutoa ushauri na mwongozo kuhusu tafsiri ya sheria kwa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi nyingine za serikali.
- Kuandaa na kutekeleza mpango wa tafsiri ya sheria kwa mwaka wa fedha na kumshauri ipasavyo Mwandishi Mkuu wa Sheria.
- Kuratibu mikutano ya ushirikishwaji wa wadau wakati wa mchakato wa tafsiri ya sheria.
- Kushauri na kusimamia uchapishaji wa sheria zilizotafsiriwa katika Gazeti la Serikali.
- Kuhakikisha usahihi na mfanano wa sheria zilizotafsiriwa kwa kuzingatia kanuni za uandishi wa sheria.
- Kuandaa, kutunza na kuendeleza rejesta ya sheria zilizotafsiriwa.