Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

Majukumu ya Kitengo cha Udhibiti Ubora

.

Kitengo kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo.

Lengo

Kuhakikisha kwamba sheria na nyaraka zinazohusiana zinazoandaliwa na Ofisi zinakidhi malengo na viwango vya usahihi,mfanano na uhalali.

Majukumu

Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kumshauri Mwandishi Mkuu wa Sheria (CPD) kuhusu viwango na ubora wa nyaraka na huduma za uandishi wa sheria.
  2. Kupitia sheria zilizohakikiwa ili kuhakikisha zinaendana na viwango na kanuni zilizowekwa za uandishi wa sheria.
  3. Kuratibu uanzishwaji na uendelezaji wa viwango na kanuni za uandishi wa sheria.
  4. Kufanya tathmini ya athari za sheria baada ya kutungwa na athari za udhibiti na usimamizi.
  5. Kuanzisha mfumo wa uhakiki ubora.
  6. Kupitia miongozo ya uandishi wa sheria na kutoa mapendekezo kwa Divisheni husika kuhusu kanuni za uandishi na maendeleo yake.
  7. Kushauri juu ya maboresho ya nyenzo na zana za uandishi wa sheria.
  8. Kufanya uhakiki wa mwisho wa nyaraka za kisheria kabla ya kuchapishwa.
  9. Kutambua na kushauri kuhusu maeneo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kuandaa, kupitia, na kuhakiki nyaraka za sheria.
  10. Kupendekeza maeneo ya maboresho na kujenga uwezo na kushauri ipasavyo kwa lengo la kuboresha ubora wa nyaraka za sheria.
  11. Kuandaa taarifa za utendaji kazi.