Vigezo na Masharti
Vigezo na Masharti yafuatayo yanasimamia matumizi yote ya tovuti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria-
Huduma zetu zinatolewa kwa sharti la kukubalika kila marekebisho ya kanuni na masharti yaliyomo na kanuni nyingine za uendeshaji, sera, notisi na taratibu zitakazochapishwa na Ofisi kila baada ya muda;
Unakubali kwamba tunaweza kuhuisha tovuti hii pamoja na huduma zetu na kanuni hizi zitatumika kwa uhuishaji wowote. Tafadhali soma makubaliano haya kwa makini kabla ya kutumia au kupata huduma zetu. Kwa kupata au kutumia sehemu yoyote ya huduma zetu, unakubali kufungwa na kanuni na masharti ya makubaliano haya. Kama hukubaliani na kanuni na masharti yote ya mkataba huu, hutaweza kupata au kutumia huduma zetu.
Marekebisho katika kanuni na masharti:
Vigezo na masharti yanaweza kubadilika wakati wowote bila ya taarifa. Nakala ya hivi karibuni ya kanuni na masharti ya Ofisi zitawekwa kwenye tovuti au zinaweza kuombwa wakati wowote kwa kuwasiliana na Ofisi.