Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

OCPD Logo

𝗠𝗪𝗔𝗡𝗔𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗠𝗞𝗨𝗨 𝗪𝗔 𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗝𝗜𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗠𝗨𝗦𝗪𝗔𝗗𝗔 𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗘𝗞𝗘𝗕𝗜𝗦𝗛𝗢 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗠𝗕𝗔𝗟𝗜𝗠𝗕𝗔𝗟𝗜

Imewekwa: 18 August, 2026
𝗠𝗪𝗔𝗡𝗔𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗠𝗞𝗨𝗨 𝗪𝗔 𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗝𝗜𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗠𝗨𝗦𝗪𝗔𝗗𝗔 𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗘𝗞𝗘𝗕𝗜𝗦𝗛𝗢 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗠𝗕𝗔𝗟𝗜𝗠𝗕𝗔𝗟𝗜

Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG), Mh. Hamza Johari, amewasilisha majibu ya Serikali leo, tarehe 18 Agosti 2026, katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichoketi kujadili maoni na mapendekezo ya Kamati kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Bill, 2026), Bungeni jijini Dodoma.

Akisoma wasilisho hilo kwaniaba ya AG, CPD Njole ametoa ufafanuzi kuhusu mapendekezo ya marekebisho yanayohusu sheria mbalimbali zinazopendekezwa kufanyiwa marekebisho kupitia Muswada huo, zikiwemo Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sura ya 116; Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287; Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288; Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura ya 283; pamoja na Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini, Sura ya 138, ambapo ufafanuzi huo ulilenga kuweka wazi hoja, madhumuni na mwelekeo wa marekebisho yaliyopendekezwa na Serikali

Mchakato huo ni sehemu ya hatua za uchambuzi wa Muswada, ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria inajadili na kutoa maoni pamoja na mapendekezo kuhusu marekebisho yanayopendekezwa, huku Serikali ikitoa majibu na ufafanuzi kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikishirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD), hatua inayolenga kuhakikisha kuwa mapendekezo hayo yanafanyiwa uchambuzi wa kina kabla ya Muswada kuendelea katika hatua zinazofuata za mchakato wa kutunga sheria.