Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

OCPD Logo

𝗠𝗜𝗦𝗪𝗔𝗗𝗔 𝗦𝗔𝗕𝗔 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗬𝗔𝗣𝗜𝗧𝗜𝗪𝗔, 𝗢𝗖𝗣𝗗 𝗬𝗔𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜 𝗠𝗖𝗛𝗔𝗞𝗔𝗧𝗢

Imewekwa: 02 November, 2026
𝗠𝗜𝗦𝗪𝗔𝗗𝗔 𝗦𝗔𝗕𝗔 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗬𝗔𝗣𝗜𝗧𝗜𝗪𝗔, 𝗢𝗖𝗣𝗗 𝗬𝗔𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜 𝗠𝗖𝗛𝗔𝗞𝗔𝗧𝗢

Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD), imeshiriki kikao cha Kamati ya Baraza la Mawaziri ya Katiba na Sheria kilichoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa lengo la kujadili na kupitia Miswada mbalimbali ya sheria.

Kikao hicho kimejadili jumla ya miswada saba inayohusu maeneo mbalimbali ya kisera na kisheria nchini, ikiwa ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 na Na. 4, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Muswada wa Sheria za Sekta ya Famasi, Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri Majini Tanzania, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Madini, pamoja na Muswada wa Sheria Zinazosimamia Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu.

Ushiriki wa OCPD katika kikao hicho ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kitaasisi katika mchakato wa Uandishi wa Sheria, kwa kutoa mchango wa kitaalamu unaolenga kuhakikisha kuwa miswada inazingatia ubora wa kisheria, ulinganifu wa masharti na madhumuni ya sera za Serikali kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata za mchakato wa kutunga sheria.