๐๐ ๐๐๐ง๐๐๐ ๐ข๐๐ฃ๐ ๐๐จ๐๐๐๐๐ง๐ ๐๐๐ง๐๐๐ ๐จ๐ง๐๐๐๐๐๐ญ๐๐๐ ๐ช๐ ๐๐๐ฅ๐ ๐ฌ๐ ๐ง๐๐๐๐ ๐ฌ๐ ๐ ๐๐๐ก๐๐๐๐๐ข ๐ฎ๐ฌ๐ฑ๐ฌ
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, ameitaka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) kujikita katika kuwezesha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza kuwa Ofisi hiyo ina nafasi muhimu katika kuhakikisha sheria zinazoandaliwa zinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya maendeleo ya Taifa.
Akizungumza wakati wa kikao na Menejimenti ya OCPD, baada ya kutembelea Ofisi hiyo na kupokelewa na Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole, Mhe. Johari amesisitiza umuhimu wa OCPD kupanua wigo wa ushiriki wake katika maboresho ya sheria kwa kushirikiana na taasisi husika kutambua maeneo yanayohitaji maboresho ya kisheria, pamoja na kujikita katika kuandaa sheria
“Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ina nafasi muhimu katika kuhakikisha sheria zinazoandaliwa zinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya maendeleo, hivyo natarajia Ofisi kujikita katika kuandaa sheria, lakini pia kushiriki kikamilifu, kwa kushirikiana na taasisi husika, katika kutambua maeneo yanayohitaji maboresho ya kisheria.”
Aidha, ameeleza umuhimu wa kuimarisha matumizi ya utafiti na tathmini ya utekelezaji wa sheria ili kuhakikisha mifumo ya kisheria.
“Ni muhimu kuimarisha matumizi ya utafiti na tathmini ya utekelezaji wa sheria ili kuhakikisha mifumo ya kisheria inachochea uwekezaji, ubunifu, matumizi ya teknolojia na maendeleo endelevu.”
Katika hatua nyingine, Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole, amewasilisha taarifa ya maendeleo ya OCPD tangu kuanzishwa kwake, akielezea utekelezaji wa majukumu, na hatua zinazochukuliwa na Ofisi katika kuimarisha uwezo wa kitaalamu wa watumishi kupitia mafunzo na fursa mbalimbali za kujengeana uwezo ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake
Vilevile, Bw. Njole alieleza juhudi za Ofisi katika kuimarisha matumizi ya mifumo ya utendaji kazi kwa lengo la kuboresha utendaji na kurahisisha michakato ya kazi, na kuwezesha kuratibu na kusimamia michakato mbalimbali ya kiutendaji kwa ufanisi zaidi.
Ziara hii imeefanyika ili kujionea maendeleo ya OCPD baada ya kuanza kutekeleza majukumu yake kama taasisi inayojitegemea kiutawala, hususan katika matumizi ya teknolojia na utaalamu katika kuandaa sheria zinazokidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa.
