Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

OCPD Logo

TUFANYE KAZI KWA UBUNIFU MKUBWA KWANI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ANAHITAJI MATOKEO ZAIDI" Mhe. Dkt. Hamza Homera

Imewekwa: 26 November, 2025
TUFANYE KAZI KWA UBUNIFU MKUBWA KWANI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ANAHITAJI MATOKEO ZAIDI" Mhe. Dkt. Hamza Homera
Novemba 26, 2025. Dodoma Hayo yamesemwa na Mhe. Dkt. Zuberi Juma Homera (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria alipofanya ziara fupi katika Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) ikiwa ni sehemu kufahamiana. Mhe. Dkt. Homera ameitaka Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya OCPD kuongeza ubunifu katika utendaji kazi kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anahitaji matokeo katika utendaji kazi. "Hiki ni kipindi ambacho Mhe. Rais anahitaji zaidi matokeo kutoka kwetu hivyo niwaombe tufanye kazi kwa ubunifu na weledi na kama kutakua na changamoto yoyote katika utekelezaji wa majukumu msisite kutushirikisha," amesema Mhe. Dkt. Homera. Mhe.Dkt. Homera ameendelea kwa kuitaka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kufanya kazi zake kwa ufanisi kwani Ofisi imebeba hatma ya maisha ya watanzania wengi. "Naomba mfanye kazi zenu kwa ufanisi mkubwa maana mmebeba maisha ya watanzania kwa kufanya marekebisho ya sheria na kuandaa miswada inayopitishwa bungeni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania," ameongeza Mhe. Dkt. Homera. Kwa upande wake Mhe. Zainab Katimba (Mb), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ametambua mchango mkubwa wa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na kuwataka kuendelea kushirikiana na wadau muhimu. "Nawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayofanya nimeona kazi zenu kwani nimepata nafasi ya kufanya kazi na nyie, vilevile nahimiza kuendelea kushirikiana na wadau muhimu ili kazi zenu ziendelee kuwa na ubora zaidi," amesema Mhe. Zainab. Akitoa taarifa ya Ofisi Bi. Rehema Katuga, Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria ameainisha majukumu yanayofanywa na Ofisi ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada kwa ajili ya kupitishwa na Bunge, kuhakiki sheria ndogo, kufanya urekebu na ufasiri wa sheria pamoja na majukumu mengine yanayohusiana na uandishi wa sheria. "Ofisi yetu ina majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada kwa ajili ya kupitishwa na bunge pamoja na kuhakiki sheria ndogo, kutafsiri sheria kuu na ndogo na kuratibu uchapishaji wa sheria kwenye gazeti la serikali," ameeleza Bi. Katuga.