OCPD YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI KWA NJIA ZA KIELEKTRONIKI
OCPD YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI KWA NJIA ZA KIELEKTRONIKI
Imewekwa: 15 December, 2025
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake, ikiwemo Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD). Dodoma. Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoongozwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), kwa niaba ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa Urekebu, Bi. Rehema Katuga, ameishukuru Serikali kwa kupatikana kwa vifaa hivyo akibainisha kuwa vitachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utendaji kazi wa Ofisi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki. “Kupatikana kwa vifaa hivi ni hatua muhimu katika safari ya Ofisi yetu ya kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA, hasa ikizingatiwa kuwa tayari tumeanza maandalizi ya kutengeneza mifumo itakayohusu uandishi wa sheria, urekebu na ufasili wa sheria,” amesema Bi. Katuga. Ameongeza kuwa vifaa hivyo vitaongeza kasi ya utekelezaji wa mipango ya kidijitali ya Ofisi na kusaidia kuongeza ufanisi, uwazi na ubora wa kazi zinazotekelezwa na OCPD kupitia matumizi ya mifumo ya kielektroniki. Makabidhiano hayo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Taasisi za Umma, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
