OCPD NA UDOM WASHIRIKIANA KUIMARISHA MITAALA YA SHERIA ILI KUENDANA NA MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA
Wataalamu kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) wamekutana na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika kikao cha pamoja kilicholenga kupata maoni ya OCPD Kuhusu mitaala ya masomo ya sheria ili kuendana na mahitaji halisi ya soko la ajira, kitaaluma na kiutendaji.
Majadiliano hayo yamejikita katika kuimarisha maudhui ya mitaala, mbinu za ufundishaji, pamoja na kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi unaokidhi soko la ajira na mazingira ya sasa ya kisheria.
Kupitia kikao hicho ambacho UDOM imewakilishwa na Mhadhiri Mwandamizi, Dkt. Ryoba Marwa pamoja na Mhadhiri Msaidizi Bw. Emmanuel Baruti, pande zote zimeonesha dhamira ya kushirikiana kwa karibu katika kuboresha mtaala wa elimu ya sheria nchini, ikiwa ni pamoja na kuoanisha nadharia na vitendo, kuzingatia mabadiliko ya sheria na sera, pamoja na kukuza utafiti na ubunifu katika taaluma ya sheria. Hatua hii inatarajiwa kuchangia upatikanaji wa wataalamu wa sheria wenye weledi na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kisheria katika jamii.
