UTENGENEZAJI WA SHERIA NDOGO KIFANI ZA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

Timu ya waandishi wa sheria, chini ya uongozi wa Bw. Eustard Ngatale, Bw. Casmir Kyuki, aliyekuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria, na Bw. Nicodemus Chuwa, Mwandishi Mkuu wa Sheria Msaidizi, ilikutana kwa ajili ya kuandaa sheria ndogo kifani za mamlaka za serikali za mitaa.
Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria imechukua hatua hii ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ambao zimekuwa zikibainishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo. Changamoto hizo zinatokana na masuala mbambali ikiwemo dosari za kiandishi, kukinzana na sheria Kuu au Katiba.
Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria imechukua jitihada za kipekee katika eneo hili kwa kuandaa Sheria Ndogo Kifani. Hizi ni sampuli ambazo zitatumika kama mfano kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuhakikisha kuwa Sheria Ndogo zote zinaendana na misingi ya kisheria na sera za kitaifa.
Lengo ni kuwa na mfumo thabiti wa kisheria unaoeleweka na kutekelezeka kwa vitendo. Aidha, kuandaliwa kwa sheria ndogo kifani hizi ni hatua muhimu katika maandalizi ya mfumo wa kiektroniki wa uandishi wa sheria utakaowezesha sheria ndogo kifani kufikiwa na mawakili wa serikali kote Nchini.